Isaiah 30:1-2

Ole Wa Taifa Kaidi

1 a Bwana asema,
“Ole kwa watoto wakaidi,
kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,
wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu,
wakilundika dhambi juu ya dhambi,
2 bwale washukao kwenda Misri
bila kutaka shauri langu,
wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,
watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.
Copyright information for SwhNEN